WANANCHI WAPONGEZA, WANASIASA NA WANAHARAKATI WASIGANA RASIMU YA KATIBA MPYA...

Makamu wa Rais, Dk Gharib Bilal (katikati) akiinua juu Rasimu ya Katiba Mpya jijini Dar es Salaam, juzi. Kushoto ni Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Jaji Joseph Warioba na Waziri Mkuu Mizengo Pinda.
Wananchi wengi wamepongeza Rasimu ya Katiba mpya, akiwamo Rais Jakaya Kikwete, huku baadhi wakionesha wasiwasi juu ya ni nani atagharimia Serikali ya Muungano hasa kutokana na mambo ya kodi kutokuwa ya Muungano.

Wengine wamependekeza nchi isiwe na marais wengi kwa madai kuwa italeta mgongano wa kiitifaki. Badala yake, wamependekeza serikali za nchi washirika wa Muungano ziongozwe na mawaziri wakuu badala ya Rais.
Wakizungumza na mwandishi kwa nyakati tofauti  jana,  wengine walipendekeza Benki Kuu iendelee kuwa moja wakisema benki kuu tatu zitaiingiza nchi katika mgogoro wa sarafu kama ilivyotokea kwa nchi za Ulaya.
Rais Jakaya Kikwete amewaomba Watanzania kuwa wastahimilivu na watulivu wakati wa kujadili mapendekezo ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba yaliyo katika Rasimu ya Katiba mpya.
Maombi hayo yamo katika salamu za Rais Jakaya Kikwete kwa Tume hiyo alizozitoa jana ambapo aliwataka wananchi kuacha jazba na hamaki wakati wa mjadala wa mapendekezo hayo yaliyotolewa juzi na Tume.
“Kama tulivyosikia na kama tutakavyosoma katika Rasimu, baadhi ya mapendekezo ya Tume yakikubaliwa yatabadili sura ya nchi yetu hususan  muundo wa Muungano wetu na jinsi ya kuendesha baadhi ya mambo yetu muhimu,” alisema Rais Kikwete.
Alisema kutokana na mabadiliko hayo, baadhi ya watu watashituka na wengine hata kuhamaki na kuhamanika na kuwaasa wasifike huko.
“Tusiikasirikie wala kuilaumu Tume ya Katiba. Tuliwapa kazi ya kusikiliza maoni na kutoa mapendekezo. Wametimiza wajibu wao.  Wajibu wetu sisi sasa ni kutoa hoja za kuboresha kilichopendekezwa kama tunacho. 
“Tushiriki kwa ukamilifu kutoa maoni yetu kwa mujibu wa utaratibu utakaowekwa na Tume. Katika kufanya hayo, naomba tuongozwe na maelekezo mazuri aliyotoa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere alipokuwa Rais kwa maofisa wa Wizara ya Mambo ya Nje baada ya nchi yetu kupata Uhuru kuwa; ‘Toa Hoja Usipige Kelele’  Nawaomba tupime na kupimwa kwa uzito wa hoja tutakazozitoa,” alisema.
Alisema ikifanyika hivyo, mchakato wa Katiba mpya utakamilika kwa salama na amani na mafanikio ya hali ya juu.  “Dunia itatupongeza, itashangaa na kutamani kuja kujifunza  kutoka kwetu.”  
Rais alimpongeza Mwenyekiti wa Tume Jaji Joseph Warioba na wajumbe kwa kazi kubwa na nzuri waliyofanya hata kupata rasimu hiyo.
 “Wanastahili shukurani na pongezi kwa sababu natambua kuwa kazi yao haikuwa rahisi hata kidogo.  Kwanza, kwamba nchi yetu ni kubwa hivyo kuzunguka karibu pande zote ni shughuli pevu. Pili, kwamba kusikiliza maelfu ya wananchi wa Tanzania waliojitokeza kutoa maoni yao kuhusu Katiba wanayoitaka ni kazi kubwa sana.
“Na hasa tunapotambua ukweli, kwamba watu wana hulka tofauti na uwezo tofauti wa kuelewa na kujieleza. Si ajabu pia kwamba katika baadhi ya maeneo walikutana na watu waliohitaji wakalimani,” alisema Rais.
Alibainisha kuwa kazi ngumu kwa Tume ilikuwa  ya  kuchambua maoni na mapendekezo yote lukuki yaliyotolewa na kuamua yale ya kupendekeza yaliyojumuishwa katika Rasimu. 
“Tunawapongeza kwa umahiri wao, kwani matokeo ya kazi yao ni ya kiwango cha hali ya juu.  Tunawapongeza kwa moyo wao wa ustahamilivu, uvumilivu, kujituma na uzalendo uliowawezesha kukamilisha kazi kwa wakati mwafaka na kwa ufanisi mkubwa,” alisema Rais.
Alihimiza kuwa sasa kazi iliyobaki ni kwa wajumbe wa Mabaraza ya Katiba.  Baada ya hapo Tume itatengeneza Rasimu ya Mwisho ya Katiba itakayofikishwa kwenye Bunge Maalumu la Katiba kwa ajili ya kujadiliwa na kufanyiwa maboresho kadri wajumbe watakavyoona inafaa.
Baada ya hapo, Rasimu ya Katiba itakayotokana na mjadala na marekebisho ya Bunge Maalumu itafikishwa kwa wananchi kwa uamuzi  wa mwisho kupitia kura ya maoni.
Alisema wakati wa kutoa maoni washiriki walitoa mapendekezo mengi na tofauti ambapo baadhi yamejumuishwa na mengine hayamo kwenye Rasimu, hivyo akaomba ambao maoni na mapendekezo yao hayamo wasifadhaike wala kukasirika. 
Alishukuru waliojitokeza kutoa maoni yao kwenye mikutano na kwa njia nyingine pamoja na maofisa wa Tume na Serikali waliofanikisha mchakato huo tangu mwanzo mpaka sasa. Alishukuru pia wabunge kwa kupitisha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba iliyowezesha kufikia hatua hii. 
Rais pia alishukuru viongozi na wanachama wa vyama vya siasa na asasi za kiraia kwa ushirikiano wao na maoni yao muhimu yaliyoboresha sheria hiyo. 
“Ndugu zetu wa vyombo vya habari nao tunawashukuru kwa kuelimisha jamii. Wote nawaomba tuendelee kushirikiana na kushikamana katika hatua zinazofuata, mpaka tutakapofikia mwisho wa safari yetu na kupata Katiba mpya inayotokana na maoni yetu na ushiriki wetu,” alisema.
Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF) Profesa Ibrahim Lipumba alisifu Rasimu lakini akasema bado kuna maeneo ambayo yanahitaji ufafanuzi na marekebisho; miongoni mwao ni kueleza Serikali ya Muungano itagharimiwa na nani.
Profesa Lipumba alisema miongoni mwa mambo saba ya Muungano ambayo yataipa Serikali ya Muungano fedha ni ushuru wa bidhaa na mapato yasiyo ya kodi yatokanayo na mambo ya Muungano. Alisema mambo hayo saba hakuna yanayoweza kuipatia Serikali hiyo fedha za kujiendesha.
Mambo hayo ni Katiba na Mamlaka ya Muungano, Ulinzi na Usalama, Uraia na Uhamiaji, Sarafu na Benki Kuu, Mambo ya Nje na Usajili wa Vyama vya Siasa. "Mambo haya ni ya kidola hayawezi kuipatia Serikali hiyo mapato ya kuiwezesha kujiendesha,” alisema.
Alisema nchi zote duniani zinaendeshwa na kodi na si ushuru, hivyo kudai kuwa Serikali ya Muungano itaendeshwa kwa ushuru unaotokana na mambo ya Muungano, hilo haliwezekani. "Huo ndio upungufu mkubwa katika Rasimu hiyo”.
Tume imetakiwa pia itolee ufafanuzi juu ya kuandikwa kwa Katiba ya Tanzania Bara  ambayo itakuwa na mambo yote ya msingi ya wananchi yasiyo kwenye Katiba ya Muungano ikizingatiwa nchi inaelekea kwenye uchaguzi mkuu miaka michache ijayo.
“Je Serikali ya Bara itapatikanaje wakati uchaguzi ni mwaka 2015?” Alihoji Profesa Lipumba na kusisitiza kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba anatakiwa kutoa ufafanuzi wa kina kuhusu suala hilo mapema.
"Niliwahi kuhadharisha, kuwa kuna njama za kusogeza uchaguzi mkuu, isije ikatokea kisingizio ikawa ni Katiba ya Tanzania Bara, maana Zanzibar tayari wana ya kwao," alisema Profesa Lipumba.
Alisema Katiba ya Bara ni muhimu kuliko ya Muungano kwa vile ndiyo inagusa mambo ya ardhi, madini , elimu na rasilimali zote za nchi ambazo zinagusa wananchi wanaotaka kujua muundo wake utakuwaje.
"Hilo Jaji hakutueleza kabisa na hakututendea haki wananchi wa Bara," alisema Profesa Lipumba akisema akiisoma Rasimu hiyo atatoa maoni mengine ya kina.
Eneo lingine ambalo alilitilia shaka ni nchi kuwa na benki kuu tatu, akisema ni hatari kwa uchumi wa nchi na kuna hatari nchi ikaingia kwenye mgogoro wa sarafu kama ilivyotokea kwa nchi za Ulaya.
Katika Rasimu inapendekezwa kuwapo Benki Kuu ya Muungano wa Tanzania itakayokuwa na wajibu wa kusimamia masuala ya sarafu na fedha za kigeni na benki za washirika wa Muungano.
Benki za Washirika  zitakuwa na jukumu la kutunza akaunti ya fedha za Serikali za kila mshirika wa Muungano na kusimamia benki za biashara katika mamlaka zao.
Kwa muundo huo kwa mujibu wa Profesa Lipumba, matatizo ya sarafu ya euro yalitokana na kukosekana kwa umoja wa kibenki na umoja wa fedha za Serikali, hivyo kusababisha mgogoro mkubwa wa sarafu hiyo.
Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk Benson Bana, alisema  Rasimu imejibu dukuduku za Watanzania; lakini akapendekeza majimbo ya uchaguzi yapunguzwe.
Alisema iwapo majimbo yote yatatoa wabunge wawili ni wazi kuwa nchi itaendelea kuwa na wabunge wengi na kubeba mzigo mkubwa kifedha. Alipendekeza majimbo yapunguzwe na badala yake wilaya ichukuliwe kuwa jimbo.
Kwa sasa katika baadhi ya wilaya kuna majimbo mawili au matatu,  jambo ambalo Dk Bana alisema kwa nchi masikini ni mzigo. Alisema majimbo mawili katika wilaya moja yaachwe kwenye maeneo ya majiji ambako kuna watu wengi kama Dar es Salaam.
Eneo lingine ambalo Dk Bana alisema bado linahitaji marekebisho ni wakuu wa nchi washirika wa Muungano. Alisema nchi kuwa na marais wengi na Makamu wa Rais wengi kutatokea matatizo ya kiitifaki.
Hivyo alipendekeza ili Rais wa Muungano awe na nguvu,  ni vema viongozi wa nchi washirika wa muungano wakawa mawaziri wakuu na kubaki na Rais mmoja mtendaji. "Hii italeta hadhi kwa kiongozi badala ya kuwa na marais watatu nchi moja."
Dk Bana alisema hata gharama za uendeshaji wa Ikulu tatu katika nchi moja ni kubwa hivyo ni lazima utafutwe utaratibu wa kupunguza gharama hizo. 
"Pamoja na upungufu huo, mambo ya kurekebisha ni machache, kwani tayari  Tume imefanya kazi kubwa na nzuri," alisema Dk Bana.
Katibu Mkuu mstaafu wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA) Nestory Ngulla, alisema kuundwa kwa  serikali tatu ni kilio cha muda mrefu cha Watanzania na kilipata kupendekezwa na tume mbalimbali ikiwamo ya Jaji Francis Nyalali na ya Jaji Robert Kisanga lakini mara zote yalipuuzwa.
Mwenyekiti wa Jukwaa la Katiba (Jukata), Deus Kibamba aliipongeza Tume kwa kuandaa Rasimu aliyosema imegusa mambo muhimu kwa maslahi ya Taifa.
Kibamba, alipongeza kazi kubwa ya Tume hiyo hasa kwa kugusa maeneo mengi ambayo awali yalikuwa yakilalamikiwa na wananchi.
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Nape Nnauye, alisema CCM ina imani kubwa na Tume na sasa inajiandaa kuunda Baraza la Katiba la Chama kwa ajili ya kuipitia ipasavyo Rasimu hiyo.
Mbunge wa Kigoma Kaskazini,  Kabwe Zitto (Chadema) alisema pamoja na Rasimu kuridhisha,  imeshindwa kugusa biashara ya kimataifa kwa kuiondoa katika masuala ya Muungano.
Hata hivyo, alisisitiza kuwa dosari hiyo inaweza kufanyiwa mabadiliko kwenye mabaraza na Bunge Maalumu la Katiba huku akiipongeza Tume.
Kuhusu umri wa mgombea urais kuanzia miaka 40 Zitto ambaye ni Naibu Katibu Mkuu Bara wa Chadema, alisema anaheshimu uamuzi wa Tume.
“Wazee wetu wamefanya kazi, wamejitahidi kadri ya uwezo wao, kuna maeneo hasa masuala ya Muungano wamefanya vizuri, kuwaondoa wabunge kuwa mawaziri hili litaongeza uwajibikaji.
Kwa upande wa Zanzibar, wananchi wametofautiana na Rasimu kwa baadhi kutofurahishwa huku wengine, hususan wafuasi wa  CCM wakishangilia.
Juzi usiku baada ya kutangazwa kwa Rasimu wafuasi wa CCM wa Maskani ya Kisonge, Michenzani walikesha wakishangilia.
Hali ilikuwa tofauti kwa wafuasi wa CUF, waliodai kuwa matakwa ya wananchi yakiwamo ya Muungano wa Mkataba utakaosababisha kuzaliwa kwa Dola ya Zanzibar huru,  yalipuuzwa.
Naibu Katibu Mkuu wa CUF Hamad Masoud alisema Rasimu haijakidhi matakwa ya wananchi wa Zanzibar ambao walitaka Dola inayojitegemea.
Masoud ambaye ni Mwakilishi wa Ole, alisema Tume ilisema inaogopa kuvunjika kwa Muungano kama itatekeleza maombi ya Muungano wa Mkataba ambapo ni kitendo kinachoonesha wazi pande mbili kutoaminiana.
Hamad alisema baadhi ya mambo ambayo yamepingwa na CUF ikiwamo idadi ya wabunge kutoka Zanzibar kuingia Bunge la Jamhuri ya Muungano kuwa 20 wakati Bara ni wabunge 50.
“CUF haijaridhishwa na Rasimu hii ambayo haitokani na matakwa ya wananchi wengi ambao wametaka Zanzibar iwe Dola inayojitegemea…Muungano huu ni wa nchi mbili huru sasa iweje Bara wabunge 50 wakati Zanzibar 20,” alihoji Hamad.
Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Vuai Ali Vuai, alisema Rasimu inatokana na maoni ya wananchi hivyo yaheshimiwe. “Sisi kwa upande wa CCM tumekuwa tukisisitiza kuhusu misingi ya Katiba itakayouhakikishia uhai Muungano wetu,” alisema.
Aidha Vuai alisema bado wananchi wana nafasi kubwa ya kutoa maoni kupitia mabaraza kwa hiyo hakuna sababu ya kutilia shaka Rasimu hiyo na kusababisha fujo.
Waziri wa kwanza wa Sheria katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Maridhiano ya Kisiasa, Hassan Nassoro Moyo alielezea kusikitishwa na matamshi ya kutotambuliwa Kamati yake ambayo alisema ilifanya kazi kubwa kuleta maridhiano na mazingira mazuri ya kisasa Zanzibar.
Ofisa Habari wa Chadema, Zanzibar, Dadi Kombo Maalim, alisema kazi kubwa sasa ipo kwa mabaraza ya Katiba kwa ajili ya kuboresha Rasimu hiyo. 
Ofisa Mwandamizi wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (Tamwa) Zanzibar,  Mzuri Issa alisema wamefurahishwa na uamuzi wa kuondolewa kwa wabunge wa viti maalumu wanawake ambao mchango wao ulikuwa haufahamiki.
Katibu wa Jumuiya ya Watu Wasioona Zanzibar (ZANAB), Adil Mohamed, alisema wamefurahishwa na Rasimu ambayo kwa mara ya kwanza imewakumbuka na kutaja watu wenye ulemavu kupewa nafasi tano za ubunge za uteuzi wa Rais.
Wabunge wakiwemo wa Viti Maalumu, wameeleza kuridhishwa na mapendekezo ya Rasimu ya Katiba ya kutaka Viti Maalumu bungeni visiwepo huku baadhi wakisema uwepo wake ulisababisha maneno mengi.
Akizungumza na mwandishi jana mjini hapa, Mbunge wa Kuteuliwa, ambaye pia ni Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi, James Mbatia ni bora viondolewe kwani baadhi ya vyama vilikuwa vikiweka watu kwa maslahi yao.
Alisema suala la kuwapa nafasi ya viti hivyo ndugu, marafiki au wapenzi wao sasa litakuwa halipo na kwamba wote waende majimboni.
"Tusiiogope rasimu hii ni nzuri na ni hatua bora kwa taifa letu, tatizo yanapokuja mabadiliko ni kawaida ya mwanadamu kuwa na hofu.
"Tusiogope gharama wala mambo mengine, naipongeza Kamati ya Katiba kwa hatua yake hiyo ya serikali tatu na mambo mengine," alisema Mbatia.
Mbunge wa Mbinga, John Komba (CCM),  pamoja kupongeza rasimu, alihadharisha uwepo wa Serikali tatu usije kutumika kuvunja Muungano. Komba pia aliunga mkono kuondolewa Viti Maalumu.
Wabunge wengine wanaounga mkono Viti Maalumu kuondolewa, ni Mbunge wa Longido, Lekule Laizer (CCM) Mbunge wa Viti Maalumu Susan Lyimo (Chadema).
"Nimefurahi Viti Maalumu kutolewa, nilitoa maoni kwenye kamati walipotuhoji, hivi viti vilikuwa vinatunyanyasa hatukuwa na mipaka, fedha za mfuko wa jimbo hatupati. Tunawakilisha  nani?” Alisema.
Naye Mbunge wa Viti Maalumu, Anna Abdallah (CCM) alipongeza hatua ya kuondolewa viti italeta heshima kwa wabunge.
Kuhusu serikali tatu, Mbunge wa Ole, Rajabu Mbarouk (CUF) alisema jambo hilo lilisubiriwa na Wazanzibari . Mbunge wa Mbulu, Mustapha Akunaay   (Chadema) alisema rasimu imekuja na majibu sasa kwani sasa Tanzania Bara inapata serikali yake.

13 comments:

Anonymous said...

I was able to find gookd information from your blog posts.

Anonymous said...

Hi, constantly i used to check blog posts here in the early hours in the morning, as i enjoy to learn more
and more.

Anonymous said...

Someone necessarily help to make severely articls I would
state. That is the first time I frequented your web
page and up to now? I surprised with the research you made to create
this actual publish amazing. Fantastic task!

Anonymous said...

Hurrah, that's what I was searching for, what a material!
existing here at this blog, thanks admin of
this web site.

Anonymous said...

I loved aas much as you'll receive carried out right here.
The sketch is tasteful, your authored material stylish.

nonetheless, you command get got an shakiness over that you wish be delivering the following.
unwell unquestionably come more formerly again as exactly the same nearly vvery often inside case you
shield this increase.

Anonymous said...

After looking over a number of the blog posts on your web page,
I seriously like your technique of writing a blog. I saved it to my bookmark site list and will be checking back soon. Take
a look at my website as well and let me know what you think.


#trungtamhuanluyenchohoanggia #donvihuanluyenchohoanggia

Xuyên suốt quá trình chiếm hữu, dụng
trung tâm huấn luyện chó chắc sẽ người tiêu dùng sẽ gặp phải những vấn đề trục trặc, khó khăn. Hiểu một cách sâu sắc được
khúc mắt đó đồng thời ước mong
được tạo điều kiện người tiêu thụ tốt nhất, Huấn luyện chó Hoàng Gia đã
triển khai system hàng ngũ tư vấn luôn sẵn sàng
phương pháp mọi mong muốn, khó hiểu từ phía người tiêu dùng.


Hoàng Gia
Website: Huanluyenchohoanggia.com.vn
Hotline:0903 151 304
Địa chỉ: 121 đường Bình Chiểu, phường Bình Chiểu, quận Thủ Đức, TP.HCM.


Tags: huan luyen cho,truong huan luyen cho,trung tam huan luyen cho,huan luyen cho tphcm,truong huan luyen cho tphcm

Anonymous said...

Hi all, here every one is sharing these know-how, therefore it's nice to read this website,
and I used to pay a quick visit this website daily.

Anonymous said...

Hello there, I believe your website could possibly be having web
browser compatibility problems. Whenever I take a look at your website in Safari,
it loiks fine however, when opening in Internet Explorer, it's got some overlappiing issues.

I simply wanted to give you a quick heads up!

Aart from that, wonderful website!

Anonymous said...

Appreciating the persistence you put into your site and
detailed information you offer. It's good to comme across a blog every once in a whilke that isn't the saje outdated rehashed information. Wonderful read!
I've bookmarked your site and I'm adding your RSS feeds to my Google account.

Anonymous said...

I need to to thank you for this good read!! I certainly loved
every bit of it. I have you bookmarked to check out new things
you post…

Anonymous said...

I am really pleased to glance at this web site posts which consists of tons of helpful information, thanks for providing
such data.

Anonymous said...

How to repair an oil painting that is folded and cracked?
My grandma was an amazing artist and she past away about 2 years ago.
My sister was in charge of making sure everyone
got some of my grandmas paintings. Well my sister
had thrown the paintings into a closet and left them there till today.

I was helping her move and found them. The frames had been smashed and they...
show more I painted all my life. I never knew how to restore.
I never cared to. I always loved my worn pictures and old frames.Paintings, pictures from everywhere I've ever been They are so beautiful to me.
Its like we grew up together or something.I know silly of me.

Anonymous said...

How do connect my Wii color cords into my Samsung Television when there is no yellow imput?
BROWSE THE Owner's Manual for the TV. If it describes placing the TV
to simply accept composite video, simply do since it says.
In any other case you will require a video converter, which will cost between $40 and $200.
No plain wire without consumer electronics, as can be found on numerous sites, will work.